Friday, April 23, 2010

Bw. Quinteen Matembo na wadau wengine wakiwa katika moja ya vikao vya harusi Maryland, Mwenge, DSM.

Wednesday, April 21, 2010


Watoto wa Njoka-Kati wakiwa kwenye pozi la picha


Kanisa Katoliki la Mpitimbi. Hapa ndio makao makuu ya Parokia yenye vigango vikubwa vya Lipaya na Namatuhi.
Shule ya Sekondari ya Mpitimbi. Ni kati ya shule zinazofanya vizuri Mkoani Ruvuma

Tuesday, April 20, 2010

wakazi wa mpitimbi

Wakazi wa kijiji hiki wengi wao ni Wangoni lakini wapo pia, ingawa wachache, Wanyasa, Wamatengo, Wabena, Wapangwa kwa kuyataja machache. Majina ya ukoo ya kina Mbawala, Komba, Nyoni, Haule, Mbena, Matembo, Mbeyu, Ngaponda, Ndauka, Kapinga, Chale, Ngonyani, Mapunda, chipeta, Kihwili, Mkinga, Mbawa, Mgomela, Nyirenda, Miti, Soko ni ya kawaida kabisa.

Wakazi hawa wanajishughulisha zaidi na kilimo. Miongoni mwa mazao wanayolima ni pamoja na mahindi, tumbaku, soya, ulezi, alizeti, nk.

Vyakula vya pekee vinavyopatikana Mpitimbi, ambavyo wanampitimbi waliopo Diaspora wanavimisi ni kikande, mawungu, mapotopoto a.k.a masuku, mapondo, mabuni, vipwete, madonga, ngumbi a.k.a mbulika, mangatungu, mafiwi nk.